Johansen Buberwa, Bukoba – Kagera.

Viongozi wa Jumuia ya Watumiaji Maji – CBUSO, pamoja na Wataalamu wa Maji Mkoa wa Kagera wemetakiwa kutibu maji, ili kuepuka magonjwa ambayo yanaweza kuleta madhara kwa watumiaji.

Akizungumza kwenye kikao cha tathimini na changamoto, Kaimu Meneja wa RUWASA Mkoani humo, Redempta Bilindaya amesema kipindi cha Mvua vyanzo vingi vya Maji huchafuka ikiwemo chemichemi ya mseleleko na Visima kuingiliwa na maji ya Mvua ambayo yamechafuliwa hivyo taratibu za usafishaji Maji zikifuatwa zitasaidia kulinda afya za watumiaji.

Amesema, “tunatakiwa kutibu maji kwa mujibu wa sheria za utibuji wa maji tulifundishwa namana ya kutibu maji kwa kiwango kinachotakiwa kwa sababu watu wanatumia yale maji wakiamini ni salama tumesikia umeingia ugonjwa wa mpya katika Mkoa wetu kinachotakiwa ni kutibu maji ili watu wabaki salama.”

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya Bukoba, Erasto Sima amewaasa Wananchi kuendelea kutunza na kulinda Miundombinu ya Maji kwani Serikali inaleta fedha nyingi za maendeleo huku akizitaka mamlaka za Maji kuwasomea Wananchi mapato na matumizi kila inapofanyika mikutano ya vijiji.

Awali akizungumza katika kikao hicho, Meneja wa RUWASA Wilaya Bukoba, Mhandisi Evaristo Mgaya ameishukuru Serikali kwa kuwapatia Watumishi wa kutosha katika ngazi mbalimbali ikiwemo Uhasibu, Mafundi, Watendaji wa Vijiji na Bodi hali iliyoongeza uwajibikaji, uadilifu na ufanisi katika kuendesha miradi ya maji Vijijini.

Benchikha: Ninaifahamu vizuri Wydad Casablanca
Simba Queens mguu sawa Ngao ya Jamii