Mshambuliaji wa mabingwa wa soka Tanzania bara Simba SC Meddie Kagere, ametangazwa na Kamati ya Tuzo ya Ligi Kuu, kuwa mchezaji Bora wa mwezi Agosti.

Kagere ametangazwa kuwa mchezaji bora wa mwezi, akiwashinda wachezaji wenzake Lukas Kikoti wa Namungo na Seif Karihe wa Lipuli.

Kagere alionyesha cheche zake mbele ya maafande wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT Tanzania) kwenye mchezo wa mzunguuko wa kwanza uliochezwa uwanja wa Uhuru, kwa kuifanya timu yake kutwaa alama tatu muhimu kwenye ushindi wa mabao matatu kwa moja, huku akifunga mabao mawili na kutoa pasi ya bao la tatu lililofungwa na Miraj Athuman.

Wakati huo huo kocha wa Ruvu Shooting Salum Shaban Mayanga, amechaguliwa kuwa Kocha Bora wa mwezi Agosti wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) msimu wa 2019/2020.

Ubora wa kocha huyo kwa mwezi Agosti, umeonekana dhidi ya makocha wengine waliongia kwenye kinyang’anyiro hicho kama, Mecky Mexime wa Kagera Sugar na Hitimana Thiery wa Namungo.

Mayanga alikiongoza kikosi chake kufanya maajabu katika mchezo wa mzunguuko wa kwanza wa ligi kuu, kwa kuwafunga Young Africans bao moja kwa sifuri, lililfungwa na mshambuliaji Sadat Mohamed.

Serikali kuwapeleka Israel wataalam 100 wa kilimo, mchakato wakamilika
Nape amuomba msamaha Rais Magufuli, asema alikuwa halali