Wachezaji Meddie Kagere na Luis Miquissone wamejiunga na wenzao jijini Arusha na kuanza mazoezi ya kujiwinda na mchezo wa mkondo wa kwanza wa awali wa Ligi ya Mabingwa Afrika, dhidi ya Plateau United ya Nigeria.

Wachezaji hao hawakua sehemu ya kikosi cha Simba SC kilichocheza dhidi ya Coastal Union Jumamosi (Novemba 21), Uwanja wa Sheikh Amri Abeid na kuibuka na ushindi wa mabao saba kwa sifuri.

Kagere na Miquissone walishindwa kujiunga wenzao mapema kwa kuwa walikuwa kwenye majukumu ya timu zao za Taifa, ziliozkua na mtihani wa kuwania tiketi ya kufuzu AFCON 2022.

Kikosi cha Simba SC kimeweka kambi jijini Arusha kikijiandaa na mchezo huo utakaopigwa mjini Jos, Nigeria mwishoni mwa juma hili, ikiwa ni mara ya kwanza kwa timu hizo kukutana.

Simba wanatarajiwa kuondoka nchini keshokutwa Jumatano, Novemba 25 tayari kwa mchezo huo utakaochezwa kati ya Novemba 27-29.

Kidato cha nne waanza mitihani leo
Sven: Coastal Union wamesafisha njia

Comments

comments