Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Ujerumani Kai Havertz, amesema hatarajii kuingia moja kwa moja kwenye kikosi cha kwanza cha Arsenal licha ya kuwa mchezaji wa tatu ghali zaidi katika historia ya klabu hiyo.

Arsenal ilimsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 kutoka Chelsea kwa mkataba ambao unaweza kufikia takribani Pauni Milioni 67.5, ikimaanisha ni Declan Rice pekee (Pauni Milioni 105 kutoka West Ham United) na Nicolas Pepe (Pauni Milioni 72 kutoka Lille) waliĆ³gharimu klabu hiyo fedha nyingi zaidi.

Havertz ameunda sehemu ya safu mpya ya wachezaji watatu pamoja na Rice na Martin Odegaard nyakati hizi za maandalizi ya msimu mpya.

“Nadhani kila mtu lazima apate nafasi yake katika timu,” alisema Havertz.

“Unacheza unapofanya mazoezi vizuri na kucheza vizuri kwenye michezo, nadhani lazima pia nitoe kila kitu katika kila mchezo, ndivyo ninavyoingia kwenye timu, sio mimi tu, bali pia kila mchezaji.

“Kwa hakika ni mtindo tofauti kabisa wa soka kuliko tulivyocheza Chelsea. Nadhani ni mtindo ambao unanifaa sana. Bila shaka huwa inachukua muda kidogo kuzoea hilo tena.”

Havertz alibadilisha nafasi mara kwa mara wakati wa ushindi wa 5-3 wa kirafiki dhidi ya Barcelona Jumatano (Julai 26) kwenye uwanja wa SoFi huko Los Angeles akihamia ubavu wa kushoto na pia kupitia katikati.

Alifunga bao dhidi ya klabu hiyo ya Katalunya na anaamini kuwa nafasi mpya ya Namba 8 katika mfumo anaopendelea Mikel Arteta wa 4-3-3 unaweza kumsaidia kugundua upya kiwango chake bora baada ya kipindi cha mchanganyiko cha miaka mitatu kule Stamford Bridge.

Licha ya kufunga bao la ushindi katika fainali ya ligi ya mabingwa Ulaya mwaka 2021 dhidi ya Manchester City, alijitahidi kupata matokeo bora baada ya kujiunga na Bayer Leverkusen, akifunga mabao 19 pekee katika michezo 91 ingawa alikuwa akicheza kama mshambuliaji wa kati mara kwa mara.

“Ninafurahia sana, kucheza nafasi hiyo kama nambari 8,” aliongeza Havertz.

“Niko kwenye mpira zaidi, nimeunganishwa zaidi kwenye mchezo. Ninafurahia sana. Nadhani nina nafasi kubwa ya kuimarika katika michezo, bado nazoea mchezo na kila kitu. Hadi sasa inafanya kazi kabisa.”

Ngoma apewa kazi ya ziada Simba SC
Kocha Geita Gold atamani TOP FOUR