Mwenyekiti wa Tume ya Taifa (NEC) Jaji Semistocles Kaijage, ameonya taasisi, watu au vikundi vya watu waliojipanga kutangaza matokeo ya uchaguzi baada ya zoezi la upigaji wa kura Oktoba 28,2020.

Amesema, kuwa kwa kufanya hivyo ni ukiukwaji wa sheria na kanuni za uchaguzi mkuu kwa mujibu wa katiba ya nchi.

Jaji Kaijage ametoa kauli hiyo zikiwa zimebakia chache kuelekea katika uchaguzi wa rais, wabunge na madiwani na kubainisha jukumu la kutangaza washindi wa uchaguzi ni la tume ya taifa pekee na si vinginevyo.

Aidha, Jaji Kaijage ametangaza zoezi la kuanza kutoa vitambulisho kwa mawakala walioteuliwa na vyama vya siasa kuanzia oktoba 21.

Watu kadhaa wauawa katika maandamano Nigeria
Van Dijk ampendekeza Fabinho Liverpool