Kaimu Balozi wa Marekani nchini Tanzania Dkt. Inmi Patterson amewasili Mkoani Kagera kwa ziara ya kikazi ya siku tatu kukagua miradi ya mbalimbali ya maendeleo katika Sekta ya Afya kitengo cha UKIMWI inayotoa huduma kwa wananchi na kufadhiliwa na nchi ya Marekani.
 
Akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti ofisini kwake mara baada ya kuwasili ametoa pole kwa wananchi wa Manispaa ya Bukoba waliokumbwa na mafuriko Mei 26, 2019 na kusema kuwa aliguswa na tukio hilo.
 
Akitaja dhumuni la ziara yake mkoani Kagera Kaimu Balozi Dkt. Patterson amesema kuwa amekuja Kagera kuona mafanikio ya miradi ya maendeleo hasa Sekta ya Afya inayofadhiliwa na Marekani kwani mkoa wa Kagera unaonekana kunafanya vizuri hasa katika upimaji wa watu waliombukizwa na Virusi Vya UKIMWI (VVU) hasa wananume, utoaji wa dawa za kufubaza nguvu za Virusi, pia wananchi kuhamasika kupima katika vituo vya afya.
 
“Nimefurahi sana kufika hapa kujionea miradi tunayoifadhili lakini kikubwa na nia yangu ni kuona maambukizi ya VVU yanashuka pia mkoa huu umebarikiwa kuwa na chakula cha kutosha lakini inaonekana udumavu wa watoto bado ni mkubwa lazima kuangalia mbele,’ amesema balozi Patterson
 
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Marco Gaguti amesema kuwa Kagera chakula si tatizo bali elimu tu kwa wananchi ambapo amesema kuwa sasa udumavu imekuwa ajenda yake na ya mkoa mzima kwa kutoa elimu juu ya lishe bora kwa wananchi.
 
Naye Mgagnga Mkuu wa Mkoa Dkt Marco Mbata amemhakikishia Kaimu Balozi Dkt. Patterson kuwa takwimu za hivi karibuni za udumavu kwa mkoa wa Kagera umeshuka kutoka asilimia 41.7 hadi asilimia 39.8 na mkoa bado unaendelea na kutoa elimu kwa wananchi kuhusu lishe bora.

Sababu Kiingereza kubaki lugha ya kufundishia elimu ya juu
Tanzania kuwa mwenyeji wa mkutano wa SADC