Jijini D’Salaam Hospitali ya Kairuki imewatangazia Umma kukanusha tuhuma zilizokuwa zikisambaa kwenye vyombo vya habari tarehe 28 Agosti, 2017 kuwa imemsababishia mgonjwa madhara ya kizazi kwa kumuachia vifaa vya kuzalishia ukeni.
Hospitali ya Kairuki inakiri kuwa iliwahi kumuhudumia mama mjamzito Khairat Shaib Omary kwa mara ya kwanza mnamo tarehe 15 disemba, 2016 ambapo mama huyo alijifungua kwa njia ya upasuaji.
Mnamo tarehe 10 julai, 2017 wakili Jonas Estomih Nkya wa kampuni ya Jonas & Associates Law Chambers aliwasilisha madai yao katika hospitali ya Kairuki.
Ambapo hospitali ya Kairuki ilikanusha kuhusika na tuhuma, madai ya Khairat Shaib Omary ambaye alifikisha madai yake katika Mahakama ya Hakimu Mkazi D’Salaam, kisutu katika kesi Namba 184 ya mwaka 2017.
-
Aadhibiwa kwa kusambaza tetesi za mke wa Rais kuolewa na Dr. Dre
-
Mjamzito aishitaki hospitali ya Kairuki kumsababishia utasa
Hivyo Kairuki imetaarifu Umma kuwa baada ya tarehe 21 Agosti 2016, Khairat alikiri katika hati zake za madai kuwa alihudumiwa na hospitali nyingine tofauti na Kairuki kama vile, Tanzania Occupational Health Service, Regency Hospital na Muhimbili Hospitali ya Taifa kwa nyakati tofauti.
Kufuatiwa na mshtaki kutofuata taratibu za mahakama katika kufungua kesi hiyo Hospitali ya Kairuki imekanusha tuhuma hizo kwani imesema hakuna ushahidi wa kutosha kudhibitisha kuhusika na tuhuma hiyo.
Aidha Hospitali ya Kairuki imeiomba Umma kupuuza tuhuma hiyo kwani hazina ukweli wowote , na imeomba radhi na kusikitika kwa usumbufu amabao umejitokeza.