Msanii wa bongo movie Frida Kajala maarufu kama Kajala amefuta tattoo iliyokuwa na herufi ‘H’, ambayo ni herufi ya kwanza katika jina la ya aliyekuwa mpenzi wake, msanii wa Bongo fleva Rajabu Kahali maarufu Harmonize.

Kupitia ukurasa wa mtandao wa Instagram wa binti yake Paula Kajala ameweka video ikimuonesha kajala akichora ua lenye ragi nyekundu katika mchoro ule wa awali ambapo umeonekana ukiwa na kofia ya kifalme, huku katikati kukiandikwa herufi H, na chini ilikua na alama ya karata ya jembe.

Kajala anakamilisha hilo leo ikiwa Harmonize alianza kuifuta tattoo ya yeye herufi ‘K’ miezi miwili iliyopita ambapo msanii huyo aliiongezea maneno yanayo someka ‘Konde Gang’.

Muguna huyooo Azam FC
Wafanyabiashara wakubali kuhama soko la Kariakoo kupisha uchunguzi na ukarabati