Mkuu wa Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro, Albinus Mgonya ameahidi kumwendeleza kimasomo Mwanafunzi aliyemaliza kidato cha Nne shule ya sekondar Mela, Rehema Papashi ambaye anatokea katika jamii ya Wafugaji wa Kimasai baada ya kushindwa kuendelea masomo kutokana na hali ya ugumu wa maisha licha ya kupata alama 29 katika matokeo yake ya kidato cha nne.

Mgonya ameyasema hayo wakati akikabidhi mnyama aina ya Kakakuona ambae aliokotwa na Baba wa Mtoto huyo aliyefamika kwa jina la Papashi Lesengai katika kijiji cha Kambala wilayani Humo.

Amesema kuwa kutokana na familia hiyo kuonesha kujali umuhimu wa elimu ameona ni vyema Serikali ikaunga mkono jitihadi zao ili kutoa hamasa kwa wafugaji wengine jamii ya Kimasai kusomesha watoto wa kike, hivyo ofsi ya Mkuu wa Wilaya itahakikisha inamsaidia binti huyo katika masomo ili atimize ndoto zake.

Maoni ya Manara usajili wa Bongo
Polisi watangaza Mwezi wa kiama kwa wahalifu