Askofu Zacharia Kakobe ametoa mtazamo tofauti na wa wazi kuhusu wagombea wanaowania nafasi ya urais kupitia vyama mbalimbali akidai kuwa hakuna msafi au mtakatifu.

Askofu Kakobe alitoa mtazamo wake alipopewa nafasi ya kuzungumza na kutoa ombi katika Mkutano Mkuu wa Chadema uliofanyika jana jijini Dar es Salaam.

“Tunazungumzia uchaguzi mkuu kana kwamba ataongoza mtu ambaye atakuwa mtakatifu jambo hilo sio kweli. Hatuchagui baba mtakatifu wa kuongoza makanisa au misikiti ya Tanzania,” alisema.

Kakobe aliongeza kuwa kama watanzania wataendelea kumtafuta kiongozi mtakatifu watasubiri sana na hawatampata bali wanatakiwa kumchagua kiongozi ambaye atasaidia kuwapigisha hatua ya kiuchumi.

Alisisitiza kuwa hakuna msafi, viongozi wote wa dunia hawana usafi kwa kuwa hakuna mtakatifu kati yao.

 

Safari Ya Dzeko Kuondoka Uingereza Imeiva
Vituko Kati Ya Mourinho Na Wenger Vyaendelea