Vinara wa Ligi Kuu, Simba SC wanaendelea kuimarisha kikosi chao kwa kuwaongeza mikataba wachezaji mwisho wa msimu huu 2020/21.

Jana Jumatatu (Juni 7), walimalizana na kipa wao namba mbili, Beno Kakolanya katika suala la kumuongeza mkataba mpya wa miaka miwili.

Mkataba wa awali wa kipa huyo ulikuwa unafikia tamati mwishoni mwa msimu huu, na ameona mahala sahihi pakuendelea kucheza soka lake ni Simba SC.

Simba SC walimsajili Kakolanya akitokea Young Africans msimu wa 2019-20.

Kakolanya amekua na changamoto ya kutopata nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha Simba SC, kufuatia uwezo mkubwa wa Aishi Manula ambaye ni chaguo la kwanza la kocha Gomes.

Rais wa Ufaransa apigwa kibao ziarani
Chanzo Yanga kumkataa Ajibu chaanikwa