Imeelezwa kuwa asilimia 95 ya wakazi katika kata ya Kakunyu wilayani Missenyi mkoani Kagera ni wahamiaji haramu.
Wahamiaji hao wameingia nchini kwaajili ya kutafuta ajira kwenye kilimo hasa kwenye mashamba ya malisho ndani ya ranchi ya Taifa.
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa wilaya hiyo, Kanali Denis Mwila wakati akitoa taarifa ya kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya kwa naibu waziri wa mambo ya ndani ya nchi, Hamad Masauni ambaye yupo kikazi mkoani Kagera.
“Ktika wilaya yetu kata ya Kakunyu watu 6,630 walisajiliwa huku raia halali wakiwa 319 tu, hivyo takribani asilimia 95 ya wakazi hao sio raia au auraia wao unamashaka” amebainisha kanali Mwila
Kutokana na taarifa hiyo, Masauni ameitaka idara ya uhamiaji na mamlaka ya vitambulisho vya Taifa (NIDA), kuongeza nguvu kazi katika wilaya ya Misanyi ili kukabiliana na wahamiaji haramu katika eneo hilo ambalo linapakana na nchi ya Rwanda.
” Kuna haja ya kuleta nguvu kazi kubwa sana katika idara ya uhamiaji na NIDA, lazima tuwe na takwimu halisi ya kila mtu aliyeko maeneo haya ambayo yanamashaka” amesema Masauni.