Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani amevunja Bodi ya Wakurugenzi ya Wakala wa Nishati Vijijini REA kutokana na kutoridhishwa na utendaji kazi wake.
Ameyasema hayo jijini Dodoma alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amesema kuwa bodi hiyo iliundwa mwaka 2017 kwa mujibu wa sheria ya wakala vijijini No.8 ya mwaka 2005.
“Kwa mujibu wa mamlaka niliyopewa chini ya kifungu 9 (3)(b) cha sheria No. 8 ya nishati vijijini ya 2005 nimeamua kuivunja bodi kwa kutengua uteuzi wa mwenyekiti pamoja na wajumbe wa bodi ya wakurugenzi ya wakala wa nishati vijijini kuanzia leo tarehe 12 novemba 2018″amesema Kalemani.
Aidha, amesema kuwa bodi nyingine itaundwa baadae kwa mujibu wa sheria ya nishati vijijini ya mwaka 2005, Bodi hiyo iliyokuwa ikiongozwa na mwenyekiti wake, Gigion Kaunda imedumu kwa muda wa mwaka mmoja baada ya mwaka jana.
-
Makampuni 15 yajitokeza kununua Korosho
-
Video: Hakuna aliyesalama, Polisi yaonyesha alipofichwa Mo Dewji
-
JPM afyekelea mbali makampuni yaliyojitokeza kununua Korosho
Hata hivyo, wajumbe wa Bodi ambao wametenguliwa ni pamoja na Mhandisi Innoceent Lwogwa, Happiness Mhina, Stella Mandago, Scholastica Jullu, Amina Chinja, Teobard Sabi na Michael Nyagoga.