Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar, Zuberi Katwila amesema atatumia mapumziko ya kalenda ya FIFA, kurekebisha makosa ya kikosi chake ambacho kinashika mkia kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Mtibwa Sugar wako mkiani mwa msimamo wakiwa na alama tano baada ya kushuka uwanjani mara tisa huku wakiwa wameshinda mchezo mmoja pekee, sare mbili na kufungwa mara tano.

Katwila amesema kuwa bado kikosi chake hakijamshawishi hivyo anaanza kuwapa mazoezi maalumu wachezaji wake kabla ya kuwakabili Azam FC Novemba 24, mwaka huu Uwanja wa Azam Complex, Dar es salaam.

“Tuko kwenye nafasi mbaya kwenye msimamo wa Ligi Kuu, tumeshinda mchezo mmoja pekee hivyo nafasi pekee ya kurekebisha mapungufu yetu ni kwenye kipindi hiki cha mapumziko ya kalenda ya FIFA

“Mipango yetu ni kukaa sawa tuweze kurejea kwenye ubora wetu, tunataka kuanza kupunguza makosa si jambo rahisi, nimeanza kuwaandaa wachezaji wangu ili tutakaparejea tuwe bora zaidi” amesema Katwila

Wawezeshaji mafunzo mtaala mpya watakiwa kuwa makini
Mlinda Lango SImba SC apata timu Brazil