Kiungo mshambuliaji wa timu ya taifa ya Crotia iliyoingia fainali na Ufaransa na kubuluzwa kwa magoli 4 kwa 2, Nikola Kalinic amekataa kupokea medali ya silva katika mashindano ya kombe la dunia 2018 akisema kuwa hastahili medali hiyo.

Kalinic ambaye alirudishwa nyumbani baada ya mechi ya kwanza ya Crotia alipokataa kufanya mabadiliko na mchezaji mwingine katika mechi waliocheza na Nigeria ame`sema kuwa hawezi kupokea medali hiyo kwani haoni alichoifanyia nchi yake katika mashindano haya ya kombe la dunia yaliyofanyika huko Russia.

Kiungo huyo mchezaji wa klabu ya Italy, Milan alikataa kufanyiwa ‘sub’ katika mechi ya kufungua kombe la dunia wakati wakicheza na Nigeria ambayo, Crotia ilifunga magori 2 huku Nigeria ikitoka kapa.

Kalinic ameikataa medali yake ya mshindi wa pili kombe la dunia akidai hakustahili heshima hiyo kutokana na utovu wa nidhamu aliouonesha kwa kocha wake, Zlatko Dalic kugoma kuingia uwanjani.

”Nilikuwa mpuuzi kuhisi nastahili kuingia mapema au kuanza kikosi cha kwanza. Hivyo medali hii sistahili kuipokea” amesema Kalinic.

 

 

.

 

Lugola aagiza wafungwa kuanza kujilisha
Chadema yasikitishwa Mbowe kutohudhuria uzinduzi wa kampeni