Rais wa shirikisho la soka nchini Zambia, Kalusha Bwalya amesema silaha pekee inayoweza kusaidia kuinua kiwango cha kandanda Afrika ni kushikisha wachezaji waliostaafu badala ya kuleta makocha kutoka mataifa ya nje.

Kinara huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Zambia alisema kiwango cha soka Afrika kinazidi kuzorota kwa sababu wenye kutengeneza msingi kutoka chini kama vile wachezaji waliostaafu wanazidi kubaguliwa.

Alitoa mfano wa timu ya taifa ya Zambia, Chipolopolo ambapo kocha wake(George Lwandamina)ni mzaliwa wan chi hiyo.

‘’Ni vyema kuwapa makocha wa nyumbani nafasi ya kuonyesha ujuzi na mbinu zao.Tabia ya kuchukua makocha wakigeni pekee inafaa ikome.

Tangu niongoze kabumbu nchini Zambia,nimekuwa katika mstari wa mbele kuhimiza wachezaji wetu wa nyumbani wapewe nafasi kuongoza kandanda’’

CCM Wapata Silaha Nyingine Dhidi Ya Lowassa
Ujerumani Wajiingiza Mashakani FIFA