Rais wa Uganda, Yoweri Kaguta Museveni, amewaambia wazi wapinzani wake kuwa hana mpango wa kuachia madaraka hivi karibuni, hivyo waachane na mawazo yao ya kuwaza kiti hicho.

Ameyasema hayo jijini Kampala nchini Uganda kwenye mkutano wa ndani wa chama ambao uliwakutanisha pamoja viongozi wa vyama vya upinzani vilivyopo Bungeni.

Amesema kuwa amefurahia mazungumzo yaliyokuwa yakiendelea kwenye mkutano huo, ambapo aliwaambia wapinzani wake kwamba hafikirii kubadilishana madaraka mpaka pale atakaporidhishwa na Ustawi na usalama wa kimkakati wa nchi za Afrika.

“Nasikia watu wanazungumzia kuachia madaraka, ni kwa namna gani watakaa kwenye umati na kumuona Museveni akikabidhi madaraka. Sidhani kama ni sahihi kusema hivyo, badala ya kuzungumzia hatma ya Afrika, mnaongelea vitu visivyo na maana, uchaguzi, nani atakuwa nani. na ndio kwasababu nilisema kama bado nina nguvu nitaendelea kutawala,” amesema Museveni.

Aidha, amesema kuwa huo ndio mtazamo wake na hatastaafu mpaka pale ambapo masuala ya muhimu ya Afrika yatakapo jadiliwa na kuwekwa sawa.

Hata hivyo, Museveni ambaye anakaribia kutimiza miaka 33 akiwa madarakani, alitamka hayo yote baada ya kauli ya Kiongozi wa chama cha kidemokrasia, Jenerali Norbet Mao, ambaye alisema ana ndoto yake siku kumuona Rais Museveni akikabidhi madaraka kwa mtu mwingine kwenye viwanja vya Kololo, jambo ambalo aliwakatisha matumaini kabisa wapinzani wake.

 

Mo Salah agusa rekodi ya Okocha akibeba tuzo ya Mchezaji Bora Afrika
Simba wajipa matumaini ya ushindi