Tarehe 19,2021, hii ni siku inayojikita kwenye orodha ya matukio makubwa kwenye historia ya taifa la Marekani.
Hii ni kufuatia makamu wa Rais wa nchi hiyo kamalla Haris kuwa mwanamke wa kwanza katika historia ya taifa hilo, kukabidhiwa mamlaka ya Rais wa nchi hiyo maarufu (Presidetial power).
Kamala Haris jana Nov 19, alikabidhiwa rasmi mamlaka ya kuwa Rais wa taifa hilo na kuhudumu kwenye nafasi hiyo kwa muda usiopungua dakika 30 au 40.
Utaratibu huu kwa nchini Marekani huja ikiwa kuna jambo la udhuru ya muhimu zaidi kwa Rais wa nchini ikiwa ya kiafya nk, historia hiyo inakwenda kuandikwa kufuatia Rais wa nchi hiyo Joe Biden kufika kwenye kituo cha afya na matibabu katika kituo cha afya cha kijeshi kiitwacho Walter Reed, ambaye huko anafanyiwa vipimo vya mwili mzima jambo ambalo hulifanya kila mwisho mwaka kutokana na umri wake kuwa umesogea kidogo.
Inaelezwa moja ya njia za vipimo hivyo ni pamoja na kuchomwa sindano ya ganzi katika kipindi atakachokuwa anapatiwa huduma hiyo na kwa mujibu wa madaktari inasemekana ikiwa binadamu anatachomwa sindano hiyo upo uwwzekani wa kupotezq uwezo wako wa kiakili kwa zaidi ya asilimia 90.