Makamu wa Rais wa Marekani, Kamala Harris hii leo Machi 31, 2023 anakamilisha ziara yake ya kikazi nchini hapa ambapo anatarajia kuelekea Zambia na kuhitimisha ziara yake akiwa Barani Afrika.

Akiwa nchini, Kamala alikutana na mwenyeji wake Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, Ikulu Dar es Salaam na kuzungumza mambo mbalimbali ikiwemo uimarishaji wa ushirikiano na mambo ya kiuchumi.

Aidha, Viongozi hao wamezungumza namna Tanzania inavyofanya vizuri kuimarisha demokrasia, na kuinua wanawake kiuchumi ambapo Kamala amempongeza Rais Samia kwa hatua mbalimbali alizochukua ikiwemo uimarishaji wa Demokrasia.

Ziara hiyo ya kiserikali, ilitokana na mwaliko wa Rais Samia wakati walipokutana jijini Washington mwaka 2022, ambayo pamoja na mambo mengine pia walizungumzia maendeleo ya uchumi na mabadiliko ya tabia nchi.

Ajali basi la Chuo Pwani: Dereva alilalamikia ubovu wa breki
Wazito wa Young Africans watua kibabe Lubumbashi