Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amekiri mtu mmoja kupigwa risasi na polisi wakati wakiwatawanya wafuasi wa Chadema walioandamana jana.
Wafuasi hao wa Chadema wakiongozwa na mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe waliandamana kuelekea ofisi ya msimamizi wa uchaguzi Jimbo la Kinondoni, Aron Kagurumjuli kudai viapo vya mawakala wa chama hicho.
Aidha, Maandamano hayo yalianzia viwanja vya Buibui Mwananyamala ulikokuwa ukifanyika mkutano wa kampeni wa Chadema na yalipofika eneo la Mkwajuni wafuasi hao walitawanywa na polisi, huku mtu mmoja aliyekuwa kwenye basi la daladala akidaiwa kupigwa risasi na kufariki dunia.
“Walizuia mabasi ya mwendo kasi, wakaanza kupiga mawe kwa hiyo kati ya risasi za hewani zilizopigwa kuwatawanya kuna moja ilimpata mtu,”amesema Kamanda Mambosasa.
-
Salum Mwalimu: Niko tayari kupoteza maisha kuliko kuibiwa kura
-
Video: Maalim Seif ana dharau ndio maana tumefikia hapa -Sakaya
-
Nchemba: Bila serikali Lissu angepoteza maisha
Hata hivyo, Kamanda Mambosasa amesema kuwa haijathibitishwa kuwa mtu huyo amefariki kwani yuko kwenye pilika pilika za uchaguzi, hivyo amesema atalifanyia kazi suala hilo baada ya kupata taarifa kamili.