Kamanda wa Jeshi la Jumuiya ya Afrika mshariki – EAC, Meja Jenerali Jeff Nyagah amejiuzulu nafasi hiyo na kuondoka nchini DRC akisema maisha yake yapo hatarini na hali iliyopo inaathiri utendakazi wake wa kazi.
Kujiuzulu kwa Nyagaya kunafuatia Barua aliyoiandika na kuifikisha kwa Katibu Mkuu wa EAC, akisema wasiojulikana wamekuwa wakichunguza mahali alipokuwa akiishi, ikiwemo kuweka kamera za siri na ndege zisizokuwa na rubani kupaa sehemu anayoishi na kufuatilia oparesheni za kikosi chake cha kijeshi.
Kamanda wa Jeshi la Jumuiya ya Afrika mshariki – EAC, Meja Jenerali Jeff Nyagah.
Amesema juhudi hizo zilianza mapema Januari 2023 na kudai pia kuna kampeni za vyombo vya Habari dhidi ya kikosi cha jeshi la EAC, ambapo wanajeshi wa Seeikali wamekuwa wakishirikiana na waasi wa M23 badala ya kuwapiga na kuwamaliza nguvu kitu ambacho ni kunyume na makubaliano.
Barua ya Nyagah pia imeeleza kuwa, Serikali ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo – DRC, imekuwa ikitaka uongozi wa Jeshi la Jumuiya ya Afrika Mashariki uwe wa kupokezana, kinyume na makubaliano.