Jeshi la Polisi Zanzibar limesema kuwa halina taarifa za kuonekana kwa mashekhe watatu wa Jumuiya ya Maimamu Zanzibar, ambao waliripotiwa kutoonekana tangu Januari 9, mwaka huu.
Hayo yamesemwa na Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Mjini Magharibi, Hassan Nassir Ali, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amesema kuwa jeshi hilo lilifanya kazi ya kuwatafuta mashekhe hao, lakini halikufanikiwa kuwaona.
“Zipo taarifa mitaani kuwa mashekhe hao wameonekana sasa nashangaa kwanini waliokuja kuripoti kuwa hawaonekani wameshindwa kuja kutoa taarifa kuwa wameonekana,” amesema Kamanda Ali
Aidha, Kamanda huyo ameiasa jamii kuacha kuchanganya mambo ya kihalifu na kisiasa kwa kuwa halileti taswira nzuri kwa jamii na taifa kwa ujumla.
Hata hivyo, Kamanda Ali ameongeza kuwa awali jeshi hilo lilipokea taarifa rasmi kutoka kwa familia na ndugu wa mashekhe hao, kuwa hawaonekani na wamepotea katika mazingira ya kutatanisha huku likihusishwa jeshi hilo kuwa ndio lililo wachukua.
-
Video: Serikali kulipa madeni ya watumishi wa umma
-
Diwani mwingine ajiuzulu na kuhamia CCM
-
Video: Musiba anatumika vibaya, siwezi kupuuza maneno yake- Yericko Nyerere