Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha, Jonathani Shana amesema kuwa tuhuma zinazoelekezwa kwake za kutumia salamu za Chama Cha Mapinduzi (CCM) huku yeye akiwa ni Afisa wa Polisi ambaye hatakiwi kujihusisha na masuala ya siasa amesema kuwa salaamu aliyoitumia haina uhusiano na chama hicho bali ni salamu yake binafsi.

Kamanda Shana amesema kuwa alialikwa kwenye kikao cha CCM kama Mjumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Arusha, ili kutoa taarifa kuhusiana na hali ya usalama huku sintofahamu kubwa ikijitokeza alipotumia kauli za Chama Cha Mapinduzi kwa kuwataka wajumbe wa mkutano huo kuitikia kauli ya kuwa ‘CCM haina kulialia’ kwa kuwa vyombo vya dola ni vyao.

“Ule ulikuwa ni mkutano wa ndani na mimi nilialikwa na Mkuu wa Mkoa kama sehemu ya Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Mkoa katika kipengele cha ulinzi na usalama, kama wanalalamika mimi nimetumia salamu ya CCM, wakaangalie Katiba ya CCM kama kuna aina hiyo ya salamu, ule ni msemo wangu, mwisho nilisema chama tawala hakina sababu ya kulialia, je ni sawa mtawala kulialia.” amesema Kamanda Shana

Hata hivyo, ameongeza kuwa kama kuna watu watasema amerudia aliyoyafanya Butiama mkoani Mara kwenye kumbukizi ya Mwalimu Nyerere, kwa kusema kuwa Mwalimu amefariki lakini chama chake hakijafa.

 

 

Uganda Cranes wasusia mazoezi wakidai malipo
Umoja wa Afrika walaani mashambulizi dhidi ya wakimbizi nchini Libya