Kamati kuu ya CCM imezima ndoto ya milionea Yusuf Manji ambaye ni diwani wa kata ya Mbagala kwa tiketi ya chama hicho, aliyetaka kuwa Meya wa jiji la Dar es Salaam.

Taarifa kutoka ndani ya kikao cha kamati kuu ya CCM zilizotolewa na chanzo kimoja cha kuaminika cha gazeti moja kubwa la kila siku, kilieleza kuwa Kamati Kuu iliyokaa jana chini ya mwenyekiti wake, Jakaya Kikwete ililiweka kando jina la Manji na diwani wa Kigamboni Henry Masaba.

Kamati hiyo iliamuru mchakato kuanza upya ambapo kwa mujibu wa Katibu wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Abilah Mihewa, mchakato mpya ulikamilika na kwamba ni madiwani wanne tu ambao walichukua fomu ya kuwania nafasi hiyo.

Aliwataja madiwani hao kuwa ni Aidan Kondo (Upanga Magharibi), Mariam Mohamed Lulida (Mchafukoge), Henry Satto Massada (Kivukoni) na Omary Yusufu Yenga (Mburahati).

Lowassa, Sumaye Kurusha Kete Zao Leo
Picha: Magufuli, Kikwete, Majaliwa, Samia wanavyofanya usafi Dar