Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Bunge imeshindwa kuwasilisha ripoti juu ya shambulio la risasi la Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu, ambayo ilitakiwa kuwasilishwa leo kabla ya Bunge halijaghailishwa

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Adadi Mohamed Rajabu ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Muheza kwa madai kuwa muda waliopewa kukamilisha ripoti hiyo ni mdogo hivyo hawakuwahi kukamilisha.

Aidha, Kamati hiyo ya Ulinzi na Usalama ya Bunge inatarajiwa kukutana kuanzia kesho ili kujadili na kuiwasilisha ripoti hiyo katika bunge lijalo litakaloanza mwezi Novemba 2017.

Hata hivyo, baada ya kutokea tukio la kushambuliwa kwa risasi Tundu Lissu,  Mbunge wa Nzega Mjini Hussein Bashe aliwasilisha hoja ya kulitaka bunge liunde kamati maalum ya kuchunguza tukio hilo ili iweze kubainika aliyefanya tukio hilo, na Spika Job Ndugai alikubali na kupitisha hoja hiyo.

Video: Nas na Nick Minaji katika mahusianao?
RC Rukwa ataka wahalifu wachomwe