Kamati maalumu ya tathmini ya ugonjwa wa corona (Covid-19) nchini imekamilisha kazi yake ambapo leo Mei 17, 2021 imekabithi ripoti hiyo kwa Rais Samia Suluhu Hassan ikiwa na jumla ya mapendekezo 19.

Itakumbukwa Aprili 6, 2021 Rais Samia alitangaza kuunda kamati hiyo ikiwa ni wiki chache baada ya kuapishwa na msisitizo ukiwa ni kupambana na ugonjwa huo kwa njia ya kisanyansi.

Akizungumza na waandishi wa habari Ikulu jijini Dar es Salaam, mwenyekiti wa kamati hiyo, Profesa Said Aboud kutoka Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (Muhas) amebainisha mapendekezo waliyoyatoa kwa Serikali.

Serikali kutoa taarifa za uwepo wa ugonjwa wa corona nchini na wataalamu wa afya watimize wajibu wao kitaalamu kwa kuzingatia weledi, miiko na maadili.

Amesema Tanzania ishiriki katika kufanya maamuzi na itekeleze maazimio ya kikanda na kimataifa, Serikali iendelee na hatua kuelekea kuruhusu matumizi huru ya chanjo dhidi ya ugonjwa wa corona.

Pamoja na mapendekezo hayo, amesema kamati huru ya kitaifa ya chanjo na mamlaka ya dawa na vifaa tiba (TMDA) ziendelee kushirikishwa katika kutoa ushauri na kudhibiti chanjo hizo.

“Kipaumbele cha utoaji wa chanjo dhidi ya Covid-19 nchini kiwe katika makundi ya wahudumu wa vituo vya kutolea huduma za afya na watumishi walio katika mstari wa mbele mathalani watumishi wa sekta ya utalii, hoteli, mipakani, viongozi wa dini na mahujaji,” amesema Profesa Aboud.

“Serikali iendelee kushirikisha wadau mbalimbali wakiwemo viongozi wa dini, wadau wa maendeleo, sekta binafsi na vyombo vya habari katika mapambano dhidi ya janga la Covid-19,” amesema Profesa Aboud.

Baada ya uchambuzi wa kina Kamati imependekeza Serikali itoe taarifa juu ya uwepo wa ugonjwa wa Covid 19 na ichukue hatua madhubuti kuimarisha hatua zote za kinga katika ngazi zote ili kuepusha wimbi la tatu la ugonjwa huo.

Kipaumbele cha utoaji wa chanjo ya Corona kiwe kwa Watumishi wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama na Wasafiri wanaokwenda nje ya Nchi, pia kufanya uhamasishaji na maandalizi ya upokeaji, usafirishaji na utoaji wa chanjo na Wananchi wawe huru kuamua kuchanja au laah.

Idris na wenzake waachiwa huru
Kipigo cha Simba SC chamgusa Masau Bwire