Serikali kupitia Baraza la Michezo la Taifa (BMT) limetangaza majina ya watu 12 wanaounda kamati itakayosimamia mchezo wa ngumi za kulipwa katika kipindi hiki ambacho katiba ya kuendesha mchezo huo ipo kwenye mchakato.

Akitangaza majina hayo kwa niaba ya waziri wa michezo, Katibu Mtendaji wa BMT, Mohamed Kiganja amesema miongoni mwa kazi watakazofanya ni pamoja na kuandaa mkutano mkuu wa uchaguzi.

Kiganja amesema mbali na jukumu hilo, chombo hicho pia kitakuwa na majukumu mengine mawili ikiwemo kulisaidia baraza hilo katika shughuli zake za kila siku kuhusu mchezo wa ngumi pamoja na kuendelea kupokea maoni kutoka kwa wadau wa ngumi za kulipwa ili kuboresha katiba yao.

Katibu huyo ametoa mwezi mmoja kuanzia Februari 8, mwaka huu kwa kamati hiyo kushirikiana na baraza kupokea na kuratibu maoni yote ya wadau kwaajili ya kuandaa mkutano huo utakaofanyika kwa siku moja.

Kamati hiyo ambayo ameiteua Mheshimiwa Waziri inajumuisha wajumbe wafuatao:-

  1. Emmanuel Saleh                                                        Mwenyekiti,
  2. Joe Anea                       Makamu Mwenyekiti,
  3. Yahya Poli                              Katibu,
  4. Habib Kinyogoli                                                Mjumbe,
  5. Rashid Matumla  Mjumbe,
  6. Anthony Ruta                                Mjumbe,
  7. Shomari Kimbau                                         Mjumbe,
  8. Killaga M.Killaga                       Mjumbe,
  9. Karama Nyilawila                       Mjumbe,
  10. Fike Wilson                       Mjumbe,
  11. Jaffar Ndame Mjumbe,
  12. Ali C. Bakari Mjumbe,

 

Kamati hii itakuwa na Majukumu yafuatayo:-

  1. Kusaidia Baraza la Michezo la Taifa Kuratibu shughuli za kila siku za Ngumi za Kulipwa Nchini Tanzania.
  2. Kupokea maoni kwa maandishi kutoka kwa wadau wa ngumi katika kipindi cha mwezi mmoja kupitia tovuti ya Baraza la Michezo la Taifa ambayo ni www.nationalsportscouncil.go.tz na tovuti ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo www.habari.go.tz
  3. Kuratibu mkutano wa kujadili Rasimu katika kipindi cha miezi miwili ili kuwapa wadau waliokosa nafasi kwa njia ya maandishi kutoa maoni yao.
  4. Kuandaa mkutano mkuu wa uchaguzi.

ZESCO wafanya mazoezi kwa siri
Serikali Yakataa Kuvunja Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima