Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii imeelezea kuridhishwa na azma ya Serikali ya kustawisha Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma – PSSSF, ikiwemo kulipa deni la michango ya watumishi kabla ya Mwaka 1999 lenye thamani ya Sh.Trilioni 2.17.

Mwenyekiti wa kamati hiyo, Fatuma Toufiq alitoa kauli hiyo wakati wa kikao cha kamati hiyo kilicholenga kupokea taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya PSSSF chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu.

Toufiq alimpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa jitihada zake za kuimarisha mfuko huo. Mnamo Desemba 15, 2021, serikali ililipa kiasi cha Sh.Bilioni 500 kati ya Sh.Bilioni 731 zilizohakikiwa kama madeni ya uwekezaji.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Prof.Joyce Ndalichako, alithibitisha azma ya serikali kuendelea kuboresha ufanisi wa mfuko huo na kusema kuwa watachukua ushauri uliotolewa na kamati hiyo kwa umakini.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Ofisi hiyo, Patrobas Katambi, alieleza kuwa serikali imeanzisha mifumo ya kisheria inayolenga kuhakikisha ustawi wa watumishi wanapostaafu.

Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, CPA Hosea Kashimba, alieleza kuwa serikali imechukua hatua kadhaa ikiwemo kuzuia uwekezaji katika maeneo yasiyo na tija na kuweka mipaka kwenye uwekezaji ili kuhakikisha ufanisi.

Kambini Young Africans kumenoga
WCF yatakiwa kuongeza kasi usajili wa Waajiri