Vikosi vya serikali ya Syria, vimeshambulia kambi za wakimbizi wa ndani katika eneo linaloshikiliwa na waasi kaskazini magharibi mwa nchi hiyo, na kuwaua takriban watu sita na kujeruhi wengine kadhaa.

Tukio hilo limetokea hii leo Novemba 6, 2022 nakushuhudiwa na watu kadhaa likiwemo shirika la Uangalizi wa Haki za Kibinadamu la Syria, lenye makao yake Uingereza.

Kambi ya wakimbizi iliyoshambuliwa hii leo nchini Syria.

Shirika hilo, limeripoti kuwa vikosi hivyo vilifyatua takriban makombora 30 kuelekea katika maeneo hayo yanayoshikiliwa na waasi, ikiwa ni pamoja na kambi ya Maram ikidaiwa kuwa pia ndege za kivita za Urusi pia zilishambulia maeneo hayo..

Miongoni mwa waliouawa ni watoto wawili na mwanamke mmoja ambapo Kituo cha redio kinachounga mkono Serikali cha Sham FM, kimeripoti kuwa vikosi vya serikali ya Syria vilishambulia ngome za kundi la Hayat Tahrir al-Sham lenye mafungamano na kundi la wanamgambo la al-Qaida.

Teachers Junction wavunja ukimya mkanganyiko taarifa za Walimu
Ajali ya Ndege Bukoba: Watatu wafariki