Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky amelaani mashambulizi mapya ya Urusi yaliohusisha makombora na ndege zisizo na rubani na kuyataja kama ugaidi dhidi ya raia.
Ndege hizo zisizo na rubani za Urusi, zimepachikwa jina la kamikaze kutokana na kuharibika baada ya kufanya shambulizi huku Rais Zelensky akiandika katika matandao wake wa Telegram kuwa “adui anaweza kushambulia miji lakini hawezi kuidhoofisha Ukraine.”
Vyombo vya usalama katika mji mkuu Kyiv, vimetoa tahadhri kwa raia na kuwataka kutafuta hifadhi katika sehemu za kujilinda na mabomu mapema iwezekananvyo.
Aidha, katika hatua nyingine mawaziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya wanakutana ambapo uvamizi wa Urusi nchini Ukraine ni miongoni mwa masuala yanayojadiliwa, huku Urusi ikiwa tayari imeshindwa kwenye uwanja wa mamapambano.