Kamishna wa Tume ya Uchaguzi Nchini Kenya IEBC, Roselyn Akombe jana alishushwa kwenye ndege aliyokuwa amepanda kwaajili ya kusafiri kuelekea nchini Marekani kwa ziara ya kikazi.
Maafisa wa Uwanja wa Ndege wa JKIA walimkamata kwa kosa la kukosa kibali cha kumruhusu kutoka nchini humo kuelekea nchini Marekani ambapo alitakiwa apate ruhusa maalum kutoka kwa mkuu wa maafisa wa umma, hivyo kupelekea kushushwa kwenye ndege aliyokuwa amepanda.
Aidha, aliendelea kushikiliwa katika kituo cha polisi cha uwanja wa ndege kabla ya ubalozi wa Marekani kuingilia kati hivyo kulazimu apelekwe katika uwanja wa ndege mwingine ndipo alipopata kibali baada kufanyika mawasiliano na mkuu wa maafisa wa umma Joseph Kinyua.
-
Odinga aapa kuweka mambo hadharani
- Mke wa Mugabe awaponyoka polisi Afrika Kusini na tuhuma za kumpiga mrembo
Kwa upande wake, Tume ya Huru ya Uchaguzi, IEBC imethibitisha kuwa Akombe alikuwa akielekea Marekani kwa ziara rasmi na anatarajiwa kurudi siku ya Jumapili Agosti 20 mwaka huu.
Hata hivyo, Akombe ni mmoja kati ya makamishna waliosimamia uchaguzi mkuu nchini Kenya ambapo rais Uhuru Kenyatta alifanikiwa kumshinda mpinzani wake mkuu kutoka muungano wa vyama vya siasa nchini humo NASA, Raila Odinga.