Afisa wa Tume ya Uchaguzi Kenya (IEBC) Dkt. Roselyn Akombe ametangaza kujiuzuru nafasi yake wiki moja kabla kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa marudio wa urais nchini humo.

Dkt. Akombe ametuma taarifa ya kujiuzuru nafasi hiyo huku akiwa jijini New York anakoishi ambapo alikuwa akifanya kazi na Shirika la Umoja wa Mataifa kabla ya kujiunga na tume huru ya Uchaguzi IEBC.

Aidha, Katika taarifa yake, Dkt. Akombe amesema kuwa marudio ya uchaguzi utakaofanyika hayaafiki matarajio ya uchaguzi ulio huru na wa haki kama uchaguzi uliofanyika kwa mara ya kwanza.

“Uamuzi wangu wa kuondoka IEBC utawasikitisha baadhi yenu, lakini si kwa sababu nilikosa kujaribu. Nilijaribu kadiri ya uwezo wangu ukizingatia hali na mazingira yaliyopo. Wakati mwingine unalazimika kusalimu amri na kuondoka hasa wakati maisha ya watu yanapokuwa hatarini, kwani tume kwa sasa imekuwa kama ni sehemu ya mzozo na vilevile iko matatani,”amesema Dkt. Akombe

Hata hivyo, Dkt Akombe alitarajiwa kuwa ni miongoni mwa kundi la maafisa waliokwenda Dubai kuchunguza uchapishaji wa makaratasi ya kupigia kura ili kuweza kuondoa malalamiko.

Video: Video ya Lissu yazua gumzo, Nassari aivimbia Takukuru
Magazeti ya Tanzania leo Oktoba 18, 2017