Uganda imesitisha kampeni zote za uchaguzi wa urais katika mji mkuu wa Kampala na wilaya nyingine 10 zenye idadi kubwa ya watu.

Msemaji wa Tume ya Uchaguzi, Paul Bukenya, amesema sababu ya kusimamisha kampeni hizo ni kutokana na ongezeko la maambukizo ya virusi vya corona.

Mgombea wa upinzani na mwanamuziki Robert Kyagulanyi maarufu kama Bobi Wine, ameibuka kuwa mshindani mkuu wa Rais Yoweri Museveni, ambaye amekuwa madarakani tangu mwaka 1986.

Hata hivyo nchi ya Uganda imepanga kufanya uchaguzi wake mkuu Januari 14, 2021.

Hata hivyo watu takribani 33,360 wameripotiwa kuwa na maambukizi ya virusi vya corona huku vifo vikiwa ni takribani 254.

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Desemba 28, 2020
Maajabu ya fenesi