Klabu ya Manchester City inahusishwa na mpango wa kumtafutia mkataba wa miaka kumi kiungo kutoka nchini Ufaransa na klabu bingwa nchini Italia, Juventus, Paul Labile Pogba katika kampuni ya Adidas.

Kwa mujibu wa jarida la Gazzetta dello Sport, mkataba huo na kampuni hiyo ya nchini Ujerumani, utakuwa na thamani ya pauni million 31, kiasi ambacho kitamfanya Pogba kuwa miongoni mwa wachezaji wenye fedha nyingi zaidi duniani.

Hata hivyo kiungo huyo mwenye umri wa miaka 22, huenda akaingia katika ugomvi wa kimkataba na kampuni ya Nike, endapo atakuubali mkataba wa kampuni ya Adidas ambao unatazamwa kama chambo wa kutaka kumnasa kwa urahisi ili akubalia kurejea mjini Manchester tena kwenye klabu yenye uhasama na klabu ambayo aliwahi kuitumikia mjini humo Man Utd.

Wakala wa Pogba, Mino Raiola, amesema bado wanaendelea na mazungumzo na kampuni ya Adidas, ili kuona uwezekano wa kuuvunja mkataba wa kampuni ya Nike ambayo kwa sasa inamdhamini Pogba.

Amesema endapo mambo yatakaa sawa, mchezaji wake atakuwa na kuwa sura ya Adidas ACE 16+ purecontrol.

Kwa sasa tetesi zinazidi kushika kasi huku zikielezea kuwa, Pogba atajiunga na Manchester City wakati kiokosi cha klabu hiyo kitakapokuwa chini ya meneja kutoka nchini Hispania, Pep Guardiola wakati wa majira ya kiangazi.

FC Bayern Munich Wamgeuzia Kibao Pep Guardiola
Luis Suárez : Sijutii Kutosajiliwa Arsenal