Klabu ya Lille ya Ufaransa na PSV ya Uholanzi zimeingia mkataba na kampuni ya kutengeneza vinywaji baridi duniani (Coca-Cola), kwa ajili ya kusambaza vinywaji kwa wachezaji na mashabiki wa klabu hizo nguli barani Ulaya.

Klabu ya Lille imekubali kuingia mkataba na kampuni hiyo kwa kuamini itanufaika pakubwa katika kujiendeleza na kuleta uhusiano wa karibu na mashabiki ambao ni wapenzi wakubwa na vinywaji vinavyozalishwa na Coca-Cola.

Mkataba wa Coca-Cola na klabu ya Lille utaanza rasmi msimu wa 2020-21 mpaka 2022-23, na utahusisha kusambazwa vinywaji kwenye uwanja wa Pierre Mauroy kwa michezo ya ligi ya Ufaransa na ile ya kimataifa.

Coca-Cola wamesema wana nia ya kuimarisha ukubwa wake katika maeneo ya kaskazini mwa Ufaransa na katika maeneo yote yanayotawaliwa na uwanja.

Mtendaji Mkuu wa Lille Marc Ingla, ameeleza dili hilo kama “Ushirikiano mkubwa wa kibiashara”.

Ukiachana na dili la Coca Cola katika nchi ya Uholanzi, Datch arm of bottlers Coca Cola European Partners (CCEP) pia wameongeza mkataba na Klabu ya PSV kwa miaka mitano, kutoka 2020-21 mpaka 2024-25.

Pande zote wamekubaliana kutaka kuongeza uzoefu mpya kwa mashabiki watakaotembelea katika uwanja wa Philips. Mara ya kwanza walijikita katika kutoa zawadi za kuondoka nazo baada ya kununua kinywaji katika baadhi ya michezo.

CCEP wana brand 15 katika soko la Uholanzi ikiwemo Coca-Cola, Fanta, Sprite, Fuze Tea, Chaudfontaine and Aquarius.

Huu ni mfano wa kuigwa kwa klabu za soka za Tanzania na kuachana na kasumba ya kufikiria kuwekeana fitna kila kukicha, hasa kwenye suala la usajili wa wachezaji.

Usajili wa Eric Garcia waleta ukakasi FC Barcelona
Manara atuma salamu Young Africans

Comments

comments