Kampuni ya TECNO mobile imetoa ofa kwa wateja wake kununua simu mpya iliyozinduliwa hivi karibuni aina ya TECNO SPARK 3 na kujishindia zawadi kemkem ikiwemo pikipiki mpya.

Ofa hiyo iliyopewa jina la boda la Spark 3 inaanzia jijini Dar es salaam kisha kuenea mikoa mingine hapo baadae na mteja atakayenunua TECNO Spark 3 kwenye maduka maalumu yenye ofa hiyo atapewa nafasi ya kuondoka na zawadi za papo kwa papo kama Power Bank yenye mAh 5000 pamoja data cable,

TECNO Spark 3 ni simu yenye uwezo mkubwa wa kupiga picha pamoja na kufanya vitu mbalimbali mitandaoni imezinduliwa takribani mwezi mmoja ikiwa ndio simu inayofanya vizuri zaidi kwa upande wa simu za kipato cha kati.

Aidha, simu hiyo ina ubora wa hali ya juu huku mtumiaji akipata nafasi ya kuhifadhi vitu vyake kwenye GB 16 za memory ya ndani na ina muonekano mzuri.

Hata hivyo,katika ofa hiyo, mshindi wa pikipiki atapatikana mwisho wa mwezi wa sita kwa njia ya bahati nasibu itakayo chezeshwa live kupitia mitandao ya kijamii ya TECNO mobile hasa Instagram katika maduka yanayopatikana Msimbazi Kariakoo na Mtaa wa Agrey lakini kwa upande wa mtaa sa Samora Posta lipo duka  la TECNO Experience centre huku upande wa mlimani Duka la TECNO smart hub,

Mahakama yatoa hati ya kumkamata Wema Sepetu
Marekani yaijibu Iran, 'Chagua moja kusuka au kunyoa?'