Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Atashasta Nditiye amesema kuwa serikali inalishughulikia suala la makato makubwa kwa watumiaji wa mitandao ya simu kutokana na malalamiko mengi yaliyoripotiwa.

Ameyasema hayo jijini Dar es salaam wakati akizungumza kwenye kipindi cha East Africa Breakfast kinachorushwa East Africa Radio kuhusiana na malalamiko ya wananchi kupanda kwa gharama za simu na kusema kuwa yeye ni miongoni mwa wahanga wa kukatwa gharama kubwa za matumizi ya simu.

Nditiye amesema kuwa ni kweli kuna malalamiko kwa wananchi kuhusu gharama za simu zimekuwa kubwa, wakati mwingine wakiweka pesa inakatwa hata kama hajaongea.

“Hata kwangu mimi nilishawahi kujiunga bando la saa moja, nikawa naongea ilipofika dakika 43, nikaambiwa bando la kuzungumza limeisha, kwa hiyo kama Serikali tumelipokea na tutalifanyia kazi.” amesema Nditiye

Hata hivyo, kuhusiana na matumizi ya simu Tanzania, Nditiye amesema kuwa kwasasa kuna watumiaji wa simu milioni 40, ambapo ni sawa na asilimia 94 ya Watanzania wote.

Video: Mkakati mpya wa 'kummaliza' Lissu wanaswa, Mengi zaidi yaibuka ajali ya moto Moro
Jumuiya ya Afrika Mashariki yakanusha wafanyakazi wake kuacha kazi