Waumini wa Dini ya Kiislam wamekumbushwa kuendelea kuishi kwa kufanya Ibada na Mambo ya Heri kama ilivyokuwa wakati wa kipindi cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ili kufikia malengo ya Mwezi huo.

Akitoa nasaha zake katika Baraza la Eid lililofanyika Viwanja vya Msikiti wa Ijumaa Kata Katoro Halmashauri ya Bukoba, Mgeni Rasmi katika shughuli hiyo Alhaji Sheikh Hashim Kamugunda Mwenyekiti wa Taawanu Islamic Foundation Tanzania, amewataka Waislam kuendelea kufanya mema kwani kumalizika kwa Ramadhan ni kipimo cha Uchamungu.

“…Ndugu zangu Waislam Mwezi Mtukufu ulikuwa Darasa kwetu, tulikuwa Darasani tukijifunza, sasa baada ya masomo hayo tunatakiwa kufanya mtihani katika yale tuliyojifunza ili kufikia malengo ya funga(saumu) ambayo ni Uchamungu..” Amesema Alhaji Kamugunda.

Aidha Alhaj Kamugunda ambaye ni Mwenyekiti wa Taawanu Nchini Tanzania ambao ndio wamiliki wa Zahanati mpya inayotarajiwa kufunguliwa hivi karibuni, kuhusu Zahanati hiyo ya Care & Cure amesema kwamba, awali ilipangwa Uzinduzi wa zahanati hiyo ufanyike Mei 03, 2022 lakini wamesogeza mbele mpaka taratibu nyingine zikamilike.

“..Tumekamilisha Taratibu zote za Vibali na Tumekwishalipia kila kitu, kinachosubiriwa ni Mamlaka kutoa Certificate (Cheti) ili tuweze kufungua Zahanati yetu itayohudumia Watu wa aina zote, bila kujali itikadi zao wala Dini zao, na Zahanati hii itakuwa ikitoa huduma ya kupima magonjwa zaidi ya 17, mashine zote za kupimia zipo tayari na wahudumu (Daktari) wamekwishafika..” amesema Kamugunda

Baraza hilo limehudhuriwa na Watu mbalimbali wakiwemo Masheikh Wakongwe na Wakufunzi pamoja na Mkurugenzi wa Taawanu International Hajat Zahra.

Hatimaye 'Range' ya Kajala yaingia Tanzania
Usitamani kuwa maarufu, tamani kuwa tajiri:Cardi B