Mshambuliaji wa pembeni kutoka DR Congo Deo Kanda amewaaga rasmi mashabiki wa klabu ya Simba, na kudhihirisha rasmi kuachana na klabu hiyo ambayo msimu ujao itatetea ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara na Kombe la Shirikisho (ASFC).

Kanda ni kati ya wachezaji waliotemwa na Simba SC, baada ya kumaliza mkataba wake wa mkopo katika klabu hiyo akitokea TP Mazembe ya nchini kwao DR Congo.

Akitumia akaunti yake ya mtandao wa kijamii, Kanda aliyeifungia Simba mabao manane aliandika kwa kuwashukuru wachezaji wenzake, uongozi mzima, mashabiki benchi la ufundi na bilionea na klabu hiyo aliye pia Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Mohammed Dewji kwa kuwa sehemu ya kikosi cha msimu uliopita.

Pia Mkongoman huyo aliitakia kila la heri Simba ikijiandaa na msimu mpya wa michuano ya Ligi Kuu na ile ya Mabingwa wa Afrika.

Mbali na Deo Kanda wachezaji wengine waliotemwa Simba ni Tairone Santos kutoka Brazili, Shiboub Sharrafeldin wa Sudan, Yusuf Mlipili na Shiza Kichuya.

Mbaroni kukutwa na dawa za kulevya
Belarus : Wapinzani wataka Rais aachie madaraka