Kanisa Katoliki Jimbo la Njombe limetoa msaada wa vifaa vya ofisi kwa ajili ya ofisi ya Mkuu wa Magereza mkoa wa Njombe vyenye thamani ya zaidi ya Milioni mbili, kwa lengo la kuunga mkono juhudi za jeshi hilo za kurekebisha tabia za wahalifu katika jamii ya wakazi wa mkoa huo.

Akizungumza kwa niaba ya Askofu wa jimbo hilo, Alferd Maluma Katibu wa askofu, Innocent Chaula, amesema kuwa Kanisa kama mdau wa kurekebisha tabia kiroho linafurahi kuona jeshi hilo pia likijitahidi kuwaongoza wanajamii walioteleza kurudi katika matendo ya kimaadili hali ambayo inawajengea heshima.

‘’Mimi nimetumwa na baba Askofu Maluma kuleta vifaa kwa ajili ya matumizi ya ofisi ya magereza Mkoa na tumefanya panapo wezekana nimeleta Viti vya kukalia Sita, Kompyuta ya mezani moja, na simu za upepo’’amesema Chaula.

Kwa upande wake, Mkuu wa Magereza Mkoa wa Njombe, Festo Ng’umbi, amelishukuru Kanisa hilo na kutumia fursa hiyo kuwaomba wadau wengine kujitokeza kuchangia ujenzi wa ofisi ya mkoa huo ili kuongeza ufanisi katika utendaji wao.

Naye Katibu Tawala Wilaya ya Njombe, Emmanuel George ameunga mkono kauli hiyo ambapo amesema kuwa wadau zaidi wanahitajika ili kuhakikisha ujenzi wa ofisi hizo unakamilika ili huduma zianze kutolewa

Kabila lenye lugha ya zamani kuliko makabila yote duniani
Nyimbo amkingia kifua Ndugai