Kanisa Katoliki limepata baraka mpya kwa namna ya kipekee mno, kwa kumtangaza Mtakatifu, Carlo Acutis mshawishi ambaye mwili wake umeoneshwa kwenye laba, jeans na sweta, katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Francis wa Assisi, Jumamosi Oktoba 10 2020, katika mji wa Assisi, jimbo la Perugia, Italia.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Vatican, Kijana huyo mdogo alijulikana sana katika jumuiya ya wakristo kutokana na kazi aliyoifanya katika kanisa kwa kutumia teknolojia mpya.

Acutis alizaliwa mjini London mwaka 1991, ambako wazazi wake walihamia kwa ajili ya kazi lakini alikulia Milan na alifariki akiwa na umri wa miaka 15 kutokana na kansa ya damu mnamo Oktoba 12, 2006.

Acutis anatunukiwa utakatifu mapema sana, tofauti na watakatifu wengine waliopita, ikiwa ni baada ya miaka 14 tu tangu kifo chake na anakuwa mwenye heri wa kwanza wa “Millenia hii ” aliyetumia mtandao kutumika katika kanisa, aliyeonesha mfano wa teknolojia inavyoweza kutumika vizuri sana katika kanisa.

Kiongozi wa Kanisa Katoliki Dunia Papa Francis amemuelezea kwa kusema kuwa “Kijana huyu mdogo alijua jinsi ya kutumia teknolojia ya mawasiliano mapya katika kuhubiri neno la Mungu, kuwasilisha maadili na uzuri wa kumtukuza Mungu”.

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Oktoba 12, 2020
Watu 18 wauawa kwenye mapambano kati ya koo mbili