Kanisa Katoliki limetoa waraka na muongozo unaopinga dhana ya kisasa juu ya utambulisho wa mapenzi ya jinsia moja.

Waraka huo wenye kurasa 31 umetolewa na uongozi wa makao makuu ya kanisa hilo uliopo jijini Vatican ambao unaelezea mafundisho, huku ukiwa na kichwa cha habari kisemacho ”Mungu aliumba Mke na mume”

Waraka huo unazungumzia mzozo wa mafundisho na kuongeza kuwa mjadala wa sasa kuhusu jinsia unaweza kupotosha dhana asilia ya jinsia na kuiyumbisha jamii kwa ujumla.

Aidha, muongozo huo umetoa wito wa kuwepo kwa mazungumzo, lakini unatoa mwongozo juu ya masuala kadhaa yakiwemo yanayohusu jamii ya watu wanaobadilisha jinsia zao, na unakosoa vikali wanasiasa kuligeuza suala hilo kuwa la kisiasa.

Waraka huo umesema kwamba utambulisho wa jinsia mara nyingi hauna msingi wowote isipokuwa ni dhana potofu ya mkanganyiko wa uhuru wa hisia za mtu na vile anavyotaka yeye kuonekana na kutambulika.

Vile vile umeendelea kusema kuwa jinsia haiamriwi na watu binafsi bali huamriwa na Mungu pekee, ” Maandiko matakatifu yamefichua busara ya Mungu ya mtindo wake wa uumbaji ,ambaye alimpatia binadamu kazi ya mwili, kazi ya mwanamme na mwanamke .”umesema Waraka huo

Hata hivyo, waraka huo umezitaka taasisi kuifundisha jamii usawa juu ya asili ya kweli ya wanadamu kwa kuzingatia elimu ya historia na tabia ya maendeleo ya binadamu kwa uwazi na kwa njia inayoaminika.

Kundi la New Ways, lenye makao yake nchini Marekani ambalo linatetea wapenzi wa jinsia moja, limesema kuwa waraka huo wa kanisa katoliki ni hatari na unaweza kuwadhuru watu waliobadilisha jinsia zao, pamoja na wapenzi wa jinsia moja wakike na wakiume.

Viongozi wa umma kutoka mikoa 12 kuchunguzwa
Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Juni 11, 2019