Wachezaji wa Kimataifa wa Simba SC Pappe Ousman Sakho na Sadio Kanoute huenda wakawa sehemu ya kikosi cha klabu hiyo kesho Jumatano (Februari 16), kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho Tanzania Bara ‘ASFC’.
Mchezo huo wa hatua ya 16 Bora, utashuhudia Mabingwa watetezi Simba SC wakipambana na Ruvu Shooting Uwanja wa Benjamin Mkapa kuanzia saa moja jioni.
Pappe Ousman Sakho na Sadio Kanoute walipata Mushkeli wa afya zao wakati wa mchezo wa kwanza wa Hatua ya Makundi ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika dhidi ya ASEC Mimosas iliyokubali kulala kwa mabao 3-1.
Wawili hao walizua taharuki kwa mashabiki wa Simba SC ambao waliamini huenda wakawa nje ya Uwanja kwa kipindi kirefu, lakini taarifa kutoka Simba SC imeondoa hofu hiyo kwa kueleza wachezaji hao wapo katika hali nzuri na wanatarajia kuanza mazoezi leo Jumanne (Septemba 15).
“Baada ya Uchunguzi wa Dakari Sakho na Kanoute wamepewa Mapumziko ya Siku Moja kabla ya Kesho kurudi Mazoezini kujiandaa na Mchezo wa Azam sports Federation Cup dhidi ya Ruvushooting utakaopigwa Jumatano hii” Imeeleza Taarifa hiyo kupitia Simba APP.
Katika mchezo dhidi ya ASEC Mimosas, Kiungo Mshambulaiji kutoka nchini Senegal Pappe Ousman Sakho aliifungia Simba SC bao la kwanza, huku Kiungo kutoka nchini Mali Sadio Kanoute alionesha kuhimili safu ya kiungo ya Mnyama.