Kansela wa Ujerumani anaemaliza muda wake Angela Merkel, amesema sauti za vijana wanaodai kuona hatua zaidi zikichukuliwa kulinda tabaka la hewa na kuepusha athari za mabadiliko ya tabianchi ni muhimu.

Katika mahojiano yake na chombo cha habari cha DW, Merkel amesema mkutano wa Galsgow wa mabadiliko ya tabianchi COP26 umeshafanikisha mengi, lakini kasi yake ni ya polepole kwa mitazamo ya vijana.

Amekiri kwamba huwa anawachochea vijana kuongeza shinikizo lao, na kwamba viongozi wanahitaji kuchangamka zaidi.

Katika Mkutano huo wa kujadili athari za mabadiliko ya tabianchi, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan aliwakumbusha nchi zilizoendelea kutoa misaada kwa nchi masikini ili kuendeleza mipango ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Young Africans na mpango wa kumsajili Chama
Waandamanaji Sudan warushiwa mabomu ya machozi