Naibu waziri wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu ameagiza kukamatwa kwa wananchi wote waliovamia na kukata miti bila kufuata taratibu za kisheria katika msitu wa hifadhi ya kijiji cha Kumbulu uliopo wilaya ya Gairo mkoani Morogoro.

Ametoa agizo hilo alipotembelea eneo hilo na kujionea uharibifu mkubwa uliofanywa na baadhi ya wananchi waliovamia msitu huo licha ya kufahamu eneo hilo lilitengwa kuwa hifadhi ya serikali ya kijiji tangu mwaka 2008.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Gairo, Siriel Nchemba amesema mgogoro huo umedumu kwa muda mrefu na hatua za ufumbuzi kwa ngazi ya wilaya zilielekea kushindikana, kutokana na vitisho kutoka kwa viongozi wa juu serikalini ambapo tayari baadhi ya viongozi wameondolewa katika nafasi zao.

Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Agosti 27, 2019
Lissu ashinda pingamizi dhidi ya serikali