Baada ya rapa Kanye West kudhihirisha kutoridhishwa na mwenendo wa namna mzazi mwenzie anavyomlea mtoto wao North West,  Hatimaye Kim Kardashiani ameshindwa kuvumilia na kuamua kufunguka kuhusu suala hilo.

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram (Insta story) Kim amesema kuwa  “mashambulizi ya mara kwa mara kutoka kwa Kanye kwenye mahojiano na kwenye mitandao ya kijamii yamekuwa ya kuumiza zaidi kuliko yeye alivyoumizwa na TikTok ya North West .”

“Kama mzazi ambaye ndiye mlezi mkuu wa watoto wetu, ninafanya kila niwezalo kumlinda binti yetu huku pia nikimruhusu kuonyesha kiwango cha ubunifu wake,” aliandika Kardashian.

Aliongeza kuwa “Talaka ni ngumu vya kutosha kwa watoto wetu mimi na Kanye, hamu ya kujaribu kudhibiti na kuendesha hali yetu vibaya na hadharani inasababisha maumivu zaidi kwa wote, sihitaji chochote ila uhusiano mzuri na wenye kutuunganisha kama wazazi wenza.”  Aliandika Kim Kardashian.

Baada ya Kum kuandika hisia zake hatimaye rapa Kanye West amejibu mapigo kwa kumuandikia ujumbe mwingine akijaribu kukosoa vikali alichokiandika Kim.

“Unamaanisha nini unaposema mtoa huduma mkuu? Amerika iliona ulivyojaribu kumficha binti yangu kwenye siku yake ya kuzaliwa kwa kutokutoa anwani ya inapofanyika shughuli, Uliniwekea ulinzi ndani ya nyumba ili kucheza na mwanangu. Kisha kunishtaki kuwa niliiba, ilibidi nipime dawa za kulevya baada ya sherehe ya Chicago na ulinishtaki kwa madai kuwa natumia dawa za kulevya, Tracy Romulus acha kumdanganya Kim hadi amekuwa namna hii.” Ameandika Kanye kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram.

Hii ni mara ya kwanza kwa siku za hivi karibuni Kim kumjibu Kanye lakini si mara ya kwanza kwa Kanye kuonesha kutofurahishwa na kitendo cha binit yake kuonekana kwenye mtamdao wa TikTok.

Katika mahojiano ya hivi karibuni na Hollywood Unlocked, Kanye alituma ujumbe wa moja kwa moja kwa Kim Kardashian na kumwambia asichapishe video za binti yao kwenye mitandao ya kijamii.

Julia Fox akanusha mahusiano kati yake na Drake
Saratani yaongezwa na mtindo wa maisha