Beki wa Kulia wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC, Shomary Salum Kapombe ataukosa Mchezo wa Mzunguuko wa 17 wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Dodoma Jiji FC utakaopigwa kesho Jumatatu (Machi 07), Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es salaam.
Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa Simba APP, Beki huyo amepewa mapumnziko ya siku tano na Madaktari wa Simba SC licha ya kuwa yupo FIT.
Juzi Ijumaa (Macho 04) Kapombe aliruhusiwa kutoka hospitali alipopelekwa usiku baada ya kuumia kwenye Mchezo wa Mzunguuko wa 16 wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Biashara United Mara.
Baada ya vipimo, Kapombe alibainika kuwa hajapata madhara yoyote ya kichwa, tofauti na ilivyotarajiwa na mashabiki wengi wa Simba SC ambao walionesha kushtushwa kuumia kwake.
Kwa Mantiki hiyo Kampombe atarudi kujiunga na wenzake wakati wa maandalizi ya mchezo wa Mzunguuko wanne wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika dhidi ya RS Berkane, utakaopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam Jumapili (Machi 13).
Simba SC itahitaji ushindi katika mchezo huo ili kujiimarisha kwenye mbio za kufuzu hatua ya Makundi ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika, baada ya kupoteza mchezo uliopita dhidi ya RS Berkane kwa kufungwa 2-0 ugenini.
Simba SC inashika nafasi ya pili katika msimamo wa Kundi D, ikiwa na alama 04 sawa na USGN ya Niger, huku ASEC Mimosas ikiburuza mkia kwa kuwa na alama 03.
RS Berkane inongoza msimamo wa kundi hilo kwa kufikisha alama 06, baada ya kushuka dimbani mara tatu, ikishinda michezo miwili na kupoteza mchezo mmoja.