Beki wa Kulia wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC Shomari Salum Kapombe amewatoa hofu Mashabiki na Wanachama wa klabu hiyo, kuhusu hali yake kuelekea mchezo wa Mzunguuko wanne wa Kundi D, Kombe la Shirikisho dhidi ya RS Berkane ya Morocco.

Kapombe alilazimika kutolewa nje ya Uwanja kwa machela wakati wa mchezo wa Mzunguuko wa 16 wa Ligi kuu Tanzania Bara dhidi ya Biashara United Mara Ijumaa (Macho 04), Uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar es salaam, baada ya kugongwa usoni.

Siku moja baadae, Daktari wa kikosi cha Simba SC, alitoa taarifa za kumpa mapumziko ya muda mfupi, baada ya kuonekana hana tatizo lolote kufutia majeraha yaliyompelekea kukosa sehemu ya mchezo dhidi ya Biashara United Mara.

Kapombe amesema: “Binafsi Mimi naweza kusema kwamba niwaondoe hofu Mashabiki na wanachama wa Simba SC, Mimi naendelea vizuri, mpaka sasa nimepata mapumziko kidogo kutokana na Daktari alivyoniambia na nina imani katika mchezo huo nitakuwepo (Rs Berkane) pamoja na kikosi “

Kapombe alikuwa sehemu ya kikosi cha Simba kilichoecheza michezo mitatu wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika, huku akiifunga ASEC Mimosas ya Ivory Coast kwenye mchezo wa Mzunguuko wa kwanza wa Kundi D, uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es salaam mwezi Februari.

Katika mchezo huo Simba SC ilichomoza na ushindi wa 3-1, kisha ikapata sare ya 1-1 dhidi ya USGN ya Niger na baadae ilipoteza dhidi ya RS Berkane kwa kufungwa 2-0.

Pablo: Jukumu la penati nimemkabidhi Chama
Biden apiga marufuku uagizaji wa mafuta Urusi