Mastaa wa Simba SC kuelekea katika tamasha kubwa la Simba Day wameapa kutoa burudani ya kutandaza soka tamu na zuri mbele ya mashabiki wao na kuwataka wajitokeaze kwa wingi kufurahia burudani ya mpira mkubwa kutoka kwao.

Simba SC katika kilele cha Simba Day wanatarajiwa kukipiga dhidi ya Power Dynamos mabingwa wa ligi kuu ya nchini Zambia kesho Jumapili (Agosti 06) kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar.

Akizungumza jijini Dar es salaam Mohammed Hussein Zimbwe amesema kuwa: “Sisi kama wachezaji jukumu letu ni kuhakikisha kuwa mashabiki wetu wanafurahi, baada ya kupata matukio makubwa mbalimbali kufurahi na wasanii kushuhudia utambulisho wetu sasa wanapata burudani ya mpira.

Mimi nafahamu kuwa Simba Day inavyokuwa mara zote vitu vingi hufanyika kuanzia asubuhi mpaka jioni kisha kinachofuata huwa ni burudani ndio maana nimewaahidi Wanasimba tutawafurahisha.”

Naye beki wa kulia, Shomari Kapombe amesema kuwa: “Kikubwa ambacho naweza kuwaahidi mashabiki wetu ni kuwapa burudani ya mpira mzuri na matokeo ya ushindi dhidi ya mpinzani wetu, Wanasimba wanafahamu kuwa sisi mara zote huwa tunafanya mambo makubwa kwa ajili yao hivyo watarajie mambo makubwa zaidi.”

Ahmed Ally: Huyu Fabrice Ngoma ni balaa
Watano wauawa Mgodini wakigombea Madini haramu