Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Solomon Mndeme anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi Katika Semina na mafunzo ya mchezo wa Karate Tanzania (GASSHUKU 2020) yatakayofanyika Ruvuma(Songea) kuanzia 04/12/2020( Ijumaa)* hadi 06/12/2020 (Jumapili).

Lengo kuu la semina na mafunzo hayo ni kuutangaza Mchezo wa Karate Tanzania pamoja na kuangalia viwango vya makarateka Nchini Tanzania,na itaongozwa na Mkufunzi mkuu wa Karate Tanzania Sensei Jerome Mhagama,pamoja na msaidizi wake Mikidadi Kilindo.

Lawrence Mapunda Kutoka kurugenzi ya Idara ya mahusiano kwa Umma ya Shirikisho la mchezo wa Karate Tanzania (JKA/WF-TZ) amesibitisha hilo,pamoja na kuwaomba wadau mbalimbali na waandishi wa Habari kusapoti mchezo huo.

Wakati huo huo Makarateka Kadhaa kutoka JKA HOME DOJO (SCORPION) iliyopo Upanga Jijini Dar es salaam,siku ya jana Jumatatu wamepandishwa Viwango pamoja kukabidhiwa Vyeti,Mara baada ya kufanya mtihani wa mchezo huo wa karate.

Kwa upande wa Semina na mafunzo hayo yanayoandaliwa na Shirikisho la mchezo wa Karate Tanzania (JKA/WF-TZ) yamekuwa yakifanyika katika mikoa mbalimbali kila mwaka baada ya mwaka jana kufanyika mkoani Morogoro,na mwaka huu mkoa wa Ruvuma utakuwa mwenyeji.

Rasmi:Dube nje wiki sita
Marekani: Jimbo La Arizona laidhinisha ushindi wa Biden